
Muller kutua Man United
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller amehusishwa na uhamisho wa Manchester United baada ya kutakiwa na nahodha wa zamani wa klabu hiyo ya Bavaria Lothar Matthaus kutafuta muda wa kucheza kwingineko.
Mshambuliaji wa Juventus Matias Soule, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Frosinone, anavutiwa na Ligi ya Premia huku Newcastle ikiongoza mbio za kumnasa Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 20.
Manchester United inaweza kuwauza kiungo wa kati wa Uingereza Jadon Sancho, 23, na kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, kwa Juventus kwa £26m pekee.
Sir Jim Ratcliffe, ambaye bado hajakamilisha mpango wa kuchukua shughuli za soka katika Manchester United, tayari yuko kwenye majadiliano kuhusu mustakabali wa mshambuliaji Mwingereza anayecheza kwa mkopo Mason Greenwood
Beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23, "amesalia kuwa mgombea" kwa uhamisho wa majira ya baridi kutoka Nice kwenda Manchester United.
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo anasema fowadi wa Ureno Joao Felix, 24, atarejea katika klabu hiyo ikiwa Barcelona wataamua kutofanya uhamisho wake wa mkopo Nou Camp kuwa wa kudumu.
Kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 18 ataongeza mshahara wake maradufu - kutoka £10,000 hadi £20,000 - ikiwa atakuwa mchezaji wa kawaida kwenye kikosi cha kwanza.
Baadhi ya wachezaji wa Everton wanaweza kuomba fidia kutoka kwa klabu hiyo kwa kupoteza mapato yao iwapo watashuka daraja, kufuatia adhabu ya pointi 10 ya Toffees kwa ukiukaji wa kanuni za fedha.
Nottingham Forest inaweza kukabiliwa na vikwazo vya uhamisho wa Januari juu ya malipo ya ada ya kuchelewa inayodaiwa na mawakala.
West Ham wanatazamiwa kutuma maombi ya kuongeza uwezo wa Uwanja wa London hadi kubeba watu 68,000 siku za mechi, jambo ambalo litaufanya kuwa uwanja wa pili kwa ukubwa katika Premier League nyuma ya Old Trafford.